DAR ES SALAAM DERBY, OKWI OR AJIBU? JIBU UNALO..! - BZONE

DAR ES SALAAM DERBY, OKWI OR AJIBU? JIBU UNALO..!

Share This
SPORTS: Mzaliwa wa Uganda na mshambuliaji wa Tanzania Ibrahim Ajibu  ni watu ambao wapo katika headlines ikitizamiwa Yanga kuwakaribisha Simba kwenye mchezo mkubwa Tanzania kwenye ligi kuu ya Tanzania bara, Vodacom Premier leaugue Jumamosi kwenye dimba la Uhuru,

Mshambuliaji wa Simba Okwi ambae anaeongoza ufungaji wa magoli akiwa  na magoli nane kwenye wiki ya saba ya ligi huku mshambuliaji wa yanga Ibrahim Ajibu hana magoli matano.

mbali na upande wao kwenye mechi kali na kubwa Tanzania na afrika mashariki Simba wapo juu ya ligi wakiwa wanaongoza kwa magoli huku wakiwa na alama sawa na Yanga na Mtibwa sugar

Kocha mkuu wa simba. Joseph Omog ameiangalia yanga kwa upande wa pili na kusema yanga ni wazuri sana na sio wa kuwabeza huku akiongezea kama tukishinda tunatakiwa kukaba kitu cha umuhimu kwetu sisi ni kushinda. Alisema Omog aliyewahi kufundisha Azam na Ac Leopards ya Congo.
Mghana James Kotei anaamini kwamba kuwabana viungo wa yanga Papy Kabamba Tshishimbi na Thaban Kamusoko ndo watakua waamuaji kwa yanga.

"Ajibu ni mchezaji mzuri lakini pale anapokuwa na mpira lakini akiwa hana mpira hawezi kututisha tunatakiwa kuwakaba Kamusoko na Tshishimbi ili yanga wasimiliki mchezo kama tuikfanya hivo tunaweza kushinda mchezo wetu"

kwa upande mwengine nahodha wa yanga Nadir Haroub canavaro alisema wanawaheshimu sana simba kwasababu wameonekana wapo vizuri msimu huu lakini tuta wadhibiti na kushinda 

Ikumbukwe simba iliwachapa 2-1 Yanga kwenye mchezo wa mzunguko wa pili kwenye ligi msimu ulio pita huku mzunguko wa kwanza wakitoka kwa sare ya 1-1.

No comments:

Post a Comment

Pages