
It’s funny sababu Wakazi ameipa jina diss track yake ‘Zillnass’ akimaanisha kuwa Billnass ndiye anayempa stress Zizi kiasi ambacho sasa anataka kuwa Bill tena. Ikumbukwe kuwa wakati anaanza muziki, Billnass alifananishwa sana na Godzilla.
Kwenye mahojiano na Sam Misago, Bill amedai kuwa hajisikii vizuri kuona watu wanahisi kuwa yeye ndio chanzo cha kupotea kwa Zilla kiasi cha kumpa stress kama wanavyosema. “Mimi siamini kama Godzilla ana stress, kwasababu Godzilla ni kati ya watu waliofanya vizuri kwa mfululizo, ana matukio mengi, ana mizizi kwenye huu muziki,” amesema Bill.
“Na bado ana nafasi kubwa, angalia namba ya watu wanaomfollow kwenye social media, yupo sana kwenye hii tasnia,” ameongeza.
Billnass amesema Zillnass ni diss track kali lakini akamuonya Wakazi kuwa Godzilla si wa kumchukulia poa. “Lakini naye [Wakazi] ajue Zilla si msanii wa kawaida.”
No comments:
Post a Comment