MONI CENTRAL ASHINDWA KUSIKILIZA USHAURI WA FAMILIA YAKE KUHUSU MUZIKI - BZONE

MONI CENTRAL ASHINDWA KUSIKILIZA USHAURI WA FAMILIA YAKE KUHUSU MUZIKI

Share This
ENTERTAIMENT: Rapa na mkali wa ngoma ya ‘Sembe Dona’ na ‘Usimsahau Mchizi’ aliyomshirikishwa na Roma ‘Moni Central Zone ameshindwa kusikiliza kauli ya Shangazi yake aliyemtaka asijihusishe tena na muziki kauli iliyoitoka katika kipindi ambacho Moni aliingia katika tukio la utekwaji tukio lililomhusisha Roma na wenzake.
Akipiga stori na Dizzim Online Moni amesema kuwa ni kweli tangu ameanza muziki hajawahi kupewa ruhusa na wakubwa wa familia kwa kuwa waliamini anaweza kufanikiwa zaidi kama atatumia elimu atakayo ipata tofauti na atakapofanya muziki. Moni ameendelea na muziki bila kujali changamoto ya shangazi yake kwa lengo la kuwahakikishia kuwa anaweza kufanikia katika kitu ambacho anakipenda.

No comments:

Post a Comment

Pages