AY na Kanumba hawakuongea miaka 3 baada ya kudai chake kwenye filamu iliyokuwa na ngoma yake (Video) - BZONE
demo-image

AY na Kanumba hawakuongea miaka 3 baada ya kudai chake kwenye filamu iliyokuwa na ngoma yake (Video)

Share This
Linapofika suala la mshiko kwa AY ushkaji unakuwa pembeni. Rapper huyo nguli alidai chake baada ya kusikia kuna wimbo wake umetumika kwenye filamu ya marehemu Steven Kanumba.

AY alimpigia simu Kanumba na Kanumba alikuwa kama anachukulia poa. Rapper huyo alienda mbali zaidi na kwenda na mwanasheria ofisini kwao kudai chake, baada ya hapo hawakuongea kwa miaka kama mitatu hivi.
AY alishangaa kuona story hii mtangazaji wa kipindi cha THE PLAYLIST Times FM, Lil Ommy anayo na ameweza kumuuliza swali kama hilo.
Kwa mara ya kwanza kwenye maisha yake ya Muziki, AY alifanyiwa Surprise ambayo hatukuja kuisahau pale ambapo Lil Ommy alipomshangaza AY kwa kumchezea sauti za dada yake akizungumzia kaka yake alivyokuwa dogo, vitu alivyokuwa akipendelea mpaka mapenzi yake na muziki, Je hadi familia yake huwa anapenda kuwaficha vitu vyake?
Pia AY alisema kuna collabo mwaka huu na Buster Rhymes, Wizkid, Alikiba na kuna collabo zingine kibao zipo ndani za Nameless, Fuse ODG na project za AY na FA zitarudi anytime soon.
Comment Using!!

No comments:

Post a Comment

Pages