Mchezaji wa Leicester City aliekataa kuchezea tena kisa kocha amemsaliti - BZONE

Mchezaji wa Leicester City aliekataa kuchezea tena kisa kocha amemsaliti

Share This
SPORTS: Staa wa soka wa timu ya soka ya Leicester City  Jose Leonardo Ulloa amerudi kwenye headlines baada ya kuonyesha kukasirishwa na kocha wake Claudio Ranieri kukiuka makubaliano yao na kusema hawezi kuichezea tena Leicester sababu Ranieri kamsaliti.
Jose Leonardo Ulloa ameeleza kuwa Ranieri alisema atamruhusu kuondoka Leicester City na kwenda kujiunga na klabu nyingine endapo itakuja mezani ofa ya kuanzia pound milioni 4 na kuendelea, cha kushangaza kocha huyo hataki kuona nyota huyo akiondoka tena.
Kocha wiki mbili zilizopita alisema kuwa kama ofa ya kati ya pound milioni 4 hadi 5 itakuja mezani ataniruhusu kuondoka lakini ninachokifahamu nikuwa ofa zilizokuja ni za kiwango hicho na zaidi lakini anazipotezea

No comments:

Post a Comment

Pages