
Nyota huyu wa Liverpool anapigania hali yake ili awe fiti kuelekea kwenye michuano ya Kombe la Dunia ambapo kwenye wiki zilizopita alipatwa na majeruhi kwenye fainali za klabu bingwa Ulaya.

Salah aliweza kubanwa bega lake na beki wa Real Madrid Sergio Ramos kwenye kipindi cha kwanza Kiev na kupatwa na majeruhi mazito ya Bega akitoka uwanjani na machozi mengi.
Beki wa kirussia Ilya Kutepov ametoa shtaka kwa kusema amihofii Salah kwenye mchezo wao na anaamini anaweza kumzuia kama akitumia mbinu alizotumia Ramos. Aliweza kusema "Salah awezi nitisha kwene mchezo wetu na unazani anazuulika vipi? ndio unatakiwa kufanya kile alichofanya Sergio Ramos kwa mfano, Ramos ametuonesha jinsi ya kumzuia Mo Salah na sisemi kwamba niliona huruma alivyofanya vile na alivoumia kwenye zile fainali."

Nyota huyu wa Misri mwenye umri wa miaka 25 ameshatua Urusi akiwa na kikosi cha Misri jana Jumapili na wanajiandaa kukutana na Uruguay kwenye mchezo wao wa kwanza ambao watacheza Ijumaa
No comments:
Post a Comment