Nini wewe Messi; Iceland watuzalishia moja kati ya Mshtuko kwenye Kombe la Dunia kwa kubana Pumzi Argentina. - BZONE

Nini wewe Messi; Iceland watuzalishia moja kati ya Mshtuko kwenye Kombe la Dunia kwa kubana Pumzi Argentina.

Share This
Iceland wamefanya kitu kikubwa sana kwenye kombe la Dunia kwenye siku ya leo kwenye historia ya soka kwa kuwabana mbavu Argentina kwa kutoka suluhu 1-1 kwenye mchezo ambao Lionel Messi alikosa nagasi ya kuwakomboa Argentina pale alipopata Penalty ambayo imeokolewa vilivyo na Hanners Por Halldorson.

Image result for argentina vs iceland

Licha ya hivyo sergio Aguero alipata nafasi ambayo iliwafanya mabingwa hawa wa mara mbili mda wote kuongoza ndani ya dakika ya 19 kwenye mchezo wa Kundi D. Mbali na hiyo Iceland ambao wamewashangaza Dunia ambapo walipoingiaga kwenye hatua ya robo fainali kwenye Euro 2016 na wametuonesha kabisa kwamba hawajakosea kuingia kwenye kombe la Dunia na walirudisha ndani ya dakika nne kupitia Alfred Finnbogason.

Related image

Argentina wamecheza wamecheza karibia wote wale nyota wao tunaowajua kwenye dimba la Spartak japo walipata baadhi ya mawimbi kwenye kushambulia ndani ya kipindi cha pili Lakini walitengeneza baadhi ya nafasi chache ambazo zilikuwa lulu kwao pia kwa Upande wa Messi ambae alipiga mkwaju afifu wa Penati ndani ya dakika ya 64.



Iceland ni Taifa dogo sana kwa wingi wa watu Duniani na ata kwenye kombe la Dunia pale uwanjani utaona ata mashabiki wao hawakuwa wengi ila kama utakumbuka hawa hawa Iceland waliwapiga Uingereza kwenye atua ya 16 kwenye michuano ya Euro 2016 hawa jamaa achana nao wanaushirikiano sana.

Image result for messi vs iceland

Vijana hawa wa Amerika Kusini walionekana wapo vizuri sana kwenye kushambulia japo walijipatia goli moja kupitia kwa Aguero na walijikuta wamebanwa sana wakiingia ndani ya chumba cha Iceland na Usije ukafikilia Iceland ni timu ambayo wanakaa nyuma tuu wanakaba ni wajanja sana hawa jamaa Total Football wanayocheza sijawahi kuiona kabisa na ndio kilichowafanya waweze kurudisha goli huku wakimuacha mlinda mlango wa Argentina Willy Caballero kukosa la Kufanya kabisa.



Baada ya Ronaldo kupiga Hat-Trick siku ya Jana macho yote yalikuwa kwa Messi leo kurudisha mapigo alipata matumaini kidogo lakini hakajikuta amewekwa katikati na mabeki wa Iceland ambao walikuwa wakishirikiana vizuri na kipa wao hapa hapa hakuna cha heshima wala nini ni kazi tu.


No comments:

Post a Comment

Pages