Jose mourinho hayupo teyari kumruhusu Anthony Martial kuondoka Manchester United msimu huu lakini anaweza akabadili mahamuzi yake kama atakutana na sharti moja tu kutoka kwa Mashetani wekundu,
Martial amekuwa na msimu mgumu sana kwenye dimba la Old Traffor ambapo amekuwa akipigania mda wa baadhi ya michezo baada ya kutua kwa Alexis Sanchez ambae amesajiliwa kwenye dirisha la usajili dogo Januari.

Ukosefu wake wa dakika umemletea matokeo ambayo yamemfanya kuweza kuachwa kwenye kikosi cha Ufaransa na Kocha wake Didier Deschamps, muwakilishi wa Martial Philipe Lamboley amechukua baadhi ya vitu kwenye atua nyingine tena akiliambia gazeti la Ufaransa RMC "Baada ya kufikilia majukumu yote Anthony anataka kuondoka Manchester United. Manchester United ni klabu kubwa yenye nguvu Duniani bado haijakutana na makubaliano yoyote na hiyo inaonesha kwamba sio muhimu kwao"
Baadhi ya vilabu vipo teyari kumsajili Martial ukijumuisha na mahasimu wa United kwenye Ligi Tottenham na wababe wa Italia Juventus. Lakini Manchester United haina ata habari ya kumuachia kinda huyu aondoke ata baada ya wakala wake kusema kama ataondoka.

Kwasasa martial amebakiwa na mwaka mmoja kwenye dili lake la Mwanzo likiwa na vipengele vya maamuzi ya kuendelea msimu ujao.
United wanatarajia kutengeneza Pauni Milioni 50 kama wataweza kumuuza Mfaransa huyu na Mashetani wekundu watataka kutumia kiasi hiki cha fedha kwajili ya kuziba pengo la Mshambuliaji huyu wa Kifaransa.

No comments:
Post a Comment