
Simba waliweza kucheza takribani michezo 28 ya Ligi bila kufungwa lakini rekodi yao ikaja kuaribiwa na Wakata miwa kutoka Kagera yani Kagera Sugar kwa kuchapwa bao 1 huku mchezaji mkongwe na pendwa kwenye klabu hii Raia wa Kiganda Okwi ambae anamabao 20 aliweza kukosa penati na kuwatia doa wana wa Msimbazi.
Simba wanaweza wakawa wamechukua ubingwa lakini wanatakiwa kujitathimini wao wenyewe na wakumbuke ilibakia theruthi watani wao wapindue ubao wa kete licha ya kujikusanyia alama 68 mimi nawakumbusha tena wakae watafakari nini watafanya kuweza kutetea ubingwa wao.

Wanaweza wakawa na siri kibao na tele kwenye kunyakua ubingwa wapkwa mara ya kwanza tokea msimu wa 2011/2012 ni miaka kadhaa imepita asee, ila kwa wao wanaweza wakaliona ili ni jepesi ila mimi binafsi nina waogopa Yanga sana kuliko ata Simba unajua ni kwanini????
Yanga wanaweza wakawa msimu huu hawakuwa vizuri kiuchumi ila Simba inabidi wajiulize hili swali walifikaje pale nafasi ya tatu na wameingiaje kwenye hatua ya makundi kombe la shirikisho? Kuwa na Uhakika kwa Simba kuingiza Bilioni nne kwa mwaka sio tatizo ilo bwana.Mimi nina wapa pongezi nyingi sana kwa Yanga kwasababu kuna funzo hapa tumelipata japo sisi tulio wengi atulijui japo sisi wanamsimbazi tunajigamba tu kwa kusema tuna kikosi kipana ah..! Ebu tukumbuke kidogo mechi kadhaa tulizo mkosa Okwi na Bocco tuu tulivokuwa tunaangaika kupata ushindi kwa tabu mwisho wake tunajikuta tunatoka Sare wee jaribu tena kwa haraka haraka kuangalia mchezo wa Kagera tukajikuta tunakufa wakati huo baadhi ya wachezaji tunaowajua na tumezoea kuwaona siku zote kwenye kikosi cha kwanza ..🤷🏾♂️ Tunatakiwa kumshukuru Mungu kwamba atukuweza kupata jeraha kwa wachezaji wetu muhimu kutokuwepo lakini tatizo liko hapa tumeandaa wale watakao kuja kuziba mapengo tunapokuwa kwenye wakati mgumu.!
Hongereni Yanga kwa hili imeweza sana kuwa na hali mbaya kiuchumi na kupata mapigo ya kuwakosa wachezaji wenu muhimu lakini bado mkafanikiwa kuwatumia makinda na kuwavusha mpaka hapa mlipokuwepo ni jambo zuri sana japo nyinyi hamlioni ila Mmetuachia swali kubwa sana kwenye vichwa vyetu je na sisi tuwaamini vijana wetu????

No comments:
Post a Comment