Unyanda Unasiri yake.! Kutana na Janda Goli kipa chipukizi kutoka Tanzania Goalkeeping Centre (TGTC) - BZONE

Unyanda Unasiri yake.! Kutana na Janda Goli kipa chipukizi kutoka Tanzania Goalkeeping Centre (TGTC)

Share This
No automatic alt text available.Tunajua kila mwanasoka hawepo uwanjani anakuwa na umuhimu wake na kazi yake lakini inaonekana hawa wote wanamtegemea Mlinda mlango nyuma mda wote na baadhi ya magoli kipa huwa wanafanya kazi uwanjani ionekane rahisi lakini inajumuisha stadi nyingi sana kutoka kwake. 

Image may contain: Janda Craj, standing and shoes

Bzone ilimfata mpaka mguuni chipukizi wako na kukutanisha na Jandashah Siraji Hussein ambae anamiaka 18 mpaka sasa tulijaribu kuongea na kutueleze baadhi ya mambo mbalimbali Golikipa anatakuwa kuwa nayo lakini alijaribu kutupa historia yake kwa ufupi.

Image may contain: 1 person, playing a sport, beach and outdoor

Janda aliweza kuanza na kutuambia kwamba kabla ya kujiunga na kituo cha Magolikipa yani Manyika Academy au (TGTC) yeye alikuwa ni golikipa wa mtaani na Shule lakini baadae akajajiunga na kituo icho nia na  dhumuni ni kwamba kupewa uzoefu wa kuwezakujakuwa Golikipa Professional.

Kabla ya yote Janda alianza kwa kusema kwanza unatakiwa kujua sheria za Ugolikipa nje ya eneo la Penati, na Golikipa siku zote anafata sheria kama wachezaji wengine, Janda aliendelea na kusema kwamba kuna vitu tofauti sana utofautisha Golikipa na watu wengine uwanajani kwanza unatakiwa kujua kuwa Jezi na vifaa vya golikipa ni tofauti kidogo.


Janda alituambia mpaka yeye kuchukua uhamuzi wa kuwa Golikipa haikuwa rahisi kwasababu yeye  hapo mwanzo kabla ya kukaa golini alishawahi kuwa mshambuliaji baada ya mda kidogo ndipo alipochukua uhamuzi wa kukaa golini baadan ya timu aliyokuwa anachezea kukosa Golikipa na kujikuta anakaa anadaka vizuri na ndipo alipochukua uhamuzi wwa kukaa golini.

Janda alimalizia kwa kusema kwamba kuwa golikipa mzuri inaiitaji kuwa na nguvu zaidi yani kimwili na kiakili lakini pamoja na subira na mazoezi kwa wingi na unaweza kuwa moja ya magolikipa wazuri ila akatuambia kwa yeye bado anaamini juu ya ndoto zake za kuja kuwa Golikipia Professional Nchini.

No comments:

Post a Comment

Pages