
Mfaransa huyu ameitisha mkutano ambao ata haukutarajiwa na watu wengi leo Mchana na kufunguka kwamba ataondoka klabuni hapo baada ya miaka miwili na nusu akiwa kama kocha.
Gwiji huyu mwenye umri wa miaka 45 amekuwa kwenye klabu kama kocha na kama mchezaji na alichoweza kusema kwamba kwa yeye binafsi ndio anaona ni mda muafaka kwake yeye kuondoka, kocha wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger, Antonio Conte na Mauricio Pochettino ni miongoni mwa kocha walioweza kutajwa awali kuwania kiti cha mfaransa huyo.
Zidane akiwa mchezaji wa zamani wa Real, Juventus pamoja na Bordeaux ilikuwa inaeleweka kabisa alikuwa chini ya Madrid mpaka 2020, akitokea kwenye kikosi B akichukua nafasi ilioachwa wazi na Rafa Benitez Januari 2016.

Zidane ameweza kushinda aslimia 70 ya michezo yake ya ligi akiwa kama kocha na amepoteza michezo minne tu pekee ya klabu bingwa Ulaya kwenye kipindi chake.
No comments:
Post a Comment