
Yanga ilianza hatua hiyo kwa kufungwa mabao 4-0 na USM Alger ya Algeria ambapo keshoJumatano itacheza na Rayon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Katika michuano hiyo, Yanga imepangwa Kundi D pamoja na USM Alger ya Algeria, Rayon Sport (Rwanda) na Gor Mahia kutoka Kenya.
Akizungumzia mikakati yake kwenye michuano hiyo, Zahera alisema: “Hatukuweza kufanya vizuri kwenye mchezo wa kwanza kutokana na kutokuwa na kikosi kamili kwa sababu wengine waligoma, nadhani mnajua, na mmesikia hilo.

“Lakini hivi sasa tunajipanga kwa mchezo ujao kuhakikisha tunashinda, tangu nimekuja hapa nimekuwa nikiwafuatilia wapinzani wetu tuliokuwa nao kundi moja, lakini kilichokuwa kinanifanya nisiweze kufanikiwa kuwaandaa vizuri wachezaji ni kutokana na wengine kukosekana.

“Hivi sasa wachezaji wangu wapo vizuri na matumaini yangu ni kuona tunafanya vizuri tukianza na mchezo huo dhidi ya Rayon hapa nyumbani.
No comments:
Post a Comment