
Inaeleweka Fergie alilalamika kutojisiki vizuri nyumbani kwake Wilmslow mjini Manchester siku ya Alhamisi kabla ya kuitwa kwa gari la wagonjwa Jana.

Baada ya hapo akapelekwa Hospitalini chini ya ulinzi mkali wa askari kwenye hospitali ya Salford Royal Hospital, mke wake Cathy ambae alimuoa mwaka 1966 na watoto wake yani Mark, Darren na Jason ilidhaniwa kwamba wanaweza wakaonekana maeneo ya Hospitali baada ya kuwa kwenye coma.

Vyanzo vya habari vinasema “Sir Alex yupo kwenye hali mbaya sana na familia yake imeshikwa na wasi wasi mkubwa sana huu ni mda mgumu sana kwao wanaomba ili aweze kulipita hili. Hawana uhakika kama anaweza akapita kwenye hili lakini wanajaribu kufanya kila liwezekanalo na matumaini yakuwa anaweza akasimama tena.

Kocha wa Doncaster Rovers Darren mwenye umri wa miaka 46 ambae ni mtoto wa Ferguson jana aliacha moja ya mchezo kwenye timu yake ambao walikuwa wanacheza na Wigan na kujiunga na familia yake.

Hali hii imeanza baada ya wili moja tu baada ya Ferguson kusimama mbele ya mashabiki 75000 kwenye dimba la Old Trafford.
GET WELL SOON FERGIE...
No comments:
Post a Comment