Pascal Gross ndio mtu pekee alieweza kuwapa goli Brighton kwenye mchezo huo pale alipopiga kichwa kwenye dakika ya 57 ya mchezo.
Manchester United wamepokea kichapo kutoka kwa wageni wote wa ligi kuu wakianza na Newcastle na Huddersfield kwenye ligi msimu huu. Mourinho kwasasa ameanza kupata wasi wasi juu ya nyota wake ambao wametokea kumuangusha hasa kwenye mchezo wa Brighton. Wameenda kwenye fainali za FA kwa muonekano huu sijui nini wataenda kufanya.
Maroune Fellaini ameshtakiwa wiki hii kuwa amefanya kosa kubwa sana kwa kutopewa ofa mpya na klabu yake ya Manchester United, Kwasasa Fellaini mshahara wa Pauni 80,000 kwa wiki pale Old Trafford na anataka dili la miaka miwili aendelee kubakia pale OT nyuma ya msimu huu lakini watu wanalalamika na kusema Bob Fella hana thamani ya kukaa United.
Bila Lukaku kwasababu anasumbuliwa na majeruhi ya Enka, Marcus Rashford anapata nafasi ya kuwa mshambuliaji , mshambuliaji huyu anapenda sana kukimbizana na mabeki lakini kwenye swala la mahamuzi anatakiwa kulifanyia kazi, tunaweza kuona ameweza kuanza na Anthonu Martial kwenye eneo la ushambuliaji huku mchezaji huyu mweenye umri wa miaka 20 akibaki nje ya chumba na mahamuzi afifu.
No comments:
Post a Comment