Tukiongelea nyuma kidogo wachezaji wote waliweza kuulizwa juu ya Bale ambae alishinda mara mbili siku ya Jumamosi pale madrid walipoibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Las Palmas lakini kwa kesho anaweza akapoteza nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza dhid ya Juventus.

Modric alinukuliwa akisema 'Gareth anafuraha sana kwa mda huu. Imekuwa ngumu sana kwenye msimu huu kwa upande wake alipokuwa akisumbuliwa na majeraha lakini anafanya mazoezi vizuri na kila mchezo anao cheza anazidi kuimalika.'

'wote tunajua nini analeta kwenye timu pale anapokuwa yupo vizuri na sawa anaoneshaga ubora wake upo wapi. Ni muhimu sana kwetu sisi anatusaidia na ndomana nasema kwanini muhimu kwetu sisi.
No comments:
Post a Comment