Jose Mourinho amemleta mtoto wake ili kufanya nae kazi Manchester United akiaanza kwenye mchezo wa Swansea huku Zuca Mourinho akiungana na baba yake kwenye benchi.Zuca Mourinho alikuwa ndani ya Tracksuit ya United iliowekwa chapa ya jina lake kwa kifupi 'ZM' huku Michael Carrick akiwekwa rasmi kwenye benchi la ufundi akiungana na Zuca Mourinho.

Mourinho Jr alishawahi kuwa kwenye academy ya Fulham akiwa kama golikipa kabla ya kupta kupata madili ya kujiunga na Chelsea na Real Madrid lakini kwasasa amechukua jicho la baba yake kwa kuanza kurithi mikoba ya baba yake akijumuishwa kwenye benchi la ufundi ndani ya United.

Baba na Mwana walisherekea kwa pamoja ushindi wa Europa ligi nchini Sweden msimu uliopita, Jose Mourinho alinukuliwa nyuma akitaka mtoto wake afate njia alizopita yeye.

Carrick pia amepandishwa juu baada ya kutangaza kuacha kucheza soka mwishoni mwa msimu huu na akiaanza kukaa pembeni ya Jose Mourinho kwenye benchi la ufundi kwenye mchezo ambao waliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Swansea magoli yakiwekwa kimiani na Romelu Lukaku pamoja na Alexis Sanchez.

Lakini Kocha huyu wa kireno amempa michezo nane ya kuweza kumjaribu Michael carrick ili kuweza kuona kiwango chake ili aweze kumuamini kwa upande mwengine mbali na ndani ya dimba.

No comments:
Post a Comment