“ATA SIELEWI KWANINI WALIKUWA WANAKATAA, LABDA KWASABABU MDA ULISHA" - BZONE
demo-image

“ATA SIELEWI KWANINI WALIKUWA WANAKATAA, LABDA KWASABABU MDA ULISHA"

Share This
Cristiano Ronaldo anasema kwamba Juventus hawakutakiwa kulaumu kabisa juu ya uhamuzi wa penati ambao umeweza kuwatoa kwenye klabu bingwa ulaya.

Real-Madrid-v-Juventus-UEFA-Champions-League-Quarter-Final-Second-Leg

Hasa pale Juve walipoonekana walipokuwa wanalazimsha robo fainali yao kuipeleka kwenye mda wa nyongeza kwenye dimba la Bernabeu. Ronaldo alichukua dhamana ya kwenda kupiga tuta lilokuwa na presha kubwa sana ili kuisaidia Real Madrid waweze kupona.

Champions-League-Quarter-Final-Second-Leg-Real-Madrid-vs-Juventus

Real Madrid walijikuta wamekula magoli matatu usiku wa jana na kufanya wawe sawa baada ya Mario Mandzukic alivoweza kupiga magoli mawili na huku Blaise Matuidi akichukua faida ya goli la tatu kwa kosa aliloweza kufanya Keylor Navas.

Juventus wametokea kuwa timu ambayo imeweza kutokea nyuma kwa magoli matatu nyuma wakiwa ugenini kwenye klabu bingwa Ulaya kwenye hatua ya mtoano.

Juventus-Italian-goalkeeper-Gianluigi-B

Lakini Mehdi Benatia alimdondasha chini Lucas Vazquez kwenye dakika ya 93 na Gianluigi Buffon akitolewa nje kwa kadi  nyekundubkwa kumzonga Refa.


“Kitu chochote kinaweza kikatokea kwenye mpira na unatakiwa kupigana mpaka tone la mwisho” Ronaldo alipokuwa akiongea na Bein Sports.

“Atukucheza vizuri lakini tumejifunza na hii itatusaidia sisi kukua zaidi. Tungeweza kushinda magoli  mengi lakini Juventus na Buffon walikuwa wapo vizuri.”

Real-Madrid-vs-Juventus-Spain-11-Apr-2018

Kwenye upande mwengine mzungusha mchezo alikuwa goli kipanwa Juventus Buffon ambae alifanya kazi kubwa sana ili kumuwezesha kibibi kizee kiendelee kuwepo kwenye mchezo kabla ya kutolewa kwenye dakika tatu za mwisho kwa kukataa tuta lilotolewa. Lakini Ronaldo aliendelea kusema.

Real-Madrid-v-Juventus-UEFA-Champions-League-Quarter-Final-Second-Leg

“Ata sielewi kwanini walikuwa wanakataa, Lucas Vazquez alidondoshwa chini kwa nyuma na kama wasingempa penati basi lile lilikuwa goli” Ronaldo aliendelea kuongeza ‘tulicheza kwa kasi sana ili tulipate goli moja tu na kwenye lile tukio nilijitahidi kujituliza mimi mwenyewe binafsi’

JE WEWE UNAZANI UHAMUZI WA REFA KWENYE ILE PENATI ULIKUWA NI SAWA?
Comment Using!!

No comments:

Post a Comment

Pages