ALI KIBA ON MOVE..TUNAANZA MOMBASA TUNAMALIZIA DAR ES SALAAM. RATIBA KAMILI YA NDOA YAWEKWA WAZI. - BZONE

ALI KIBA ON MOVE..TUNAANZA MOMBASA TUNAMALIZIA DAR ES SALAAM. RATIBA KAMILI YA NDOA YAWEKWA WAZI.

Share This
 Alikiba amesafiri pamoja na familia yake Jumanne hii April 17, 2018 kuelekea mjini Mombasa nchini Kenya kwaajili ya kufunga ndoa na mpenzi wake, Aminah Rikesh itayofanyika April 26, 2018 katika ukumbi wa Diamond Jubilee wa nchini humo.



Taarifa za ndoa yake ziligubikwa na usiri mkubwa hali ambayo ilivifanya vyombo vingi vya habari nchini Tanzania na Uganda kuandika tetesi za ndoa hiyo huku vingine vikienda mbali zaidi kwa kudai ndoa hiyo ilishafungwa.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, ndoa hiyo itarushwa live na kituo cha runinga cha Azam TV , Muimbaji huyo atafanya sherehe nyingine nchini Tanzania wiki moja baada ya ndoa ya awali.
Chanzo hicho kimedai ndoa hiyo itagharimu mamilioni ya hela kutokana na maandalizi pamoja na deal hilo la Azam.


No comments:

Post a Comment

Pages