'VITU VIZURI HUWA VINAMWISHO WAKE' RASMI MANCHESTER UNITED WAMEVUNJA MKATABA WAO NA ZLATAN IBRAHIMOVIC.. - BZONE

'VITU VIZURI HUWA VINAMWISHO WAKE' RASMI MANCHESTER UNITED WAMEVUNJA MKATABA WAO NA ZLATAN IBRAHIMOVIC..

Share This
Mda wa Zlatan Ibrahimovic ndani ya United umeisha baada ya mkataba wake kuvunjika. Msweden huyuu ameweza kufurahia maisha yake pale alipokuwa Manchester United  kabla ya kupata majeraha ya goti ambayo yalimueka nje kwa mda mrefu.



'Vitu vizuri huwa vinakuaga na mwisho pia ni mda muafaka wa mimi kusonga mbele baada ya misimu miwili ilio mizuri kwangu mimi nikiwa na Manchester United,' Ibrahimovic alivoweka post yake kwenye ukurasa wa Instagram.


'Ahsante sana klabu, mashabiki, timu, kocha, wafanya kazi wote wa United na kila aliekuwa pamoja na mimi kwa kila jambo kwenye sehemu hii ya historia yangu.'

Zlatan Ibrahimovic has left Manchester United after having his contract terminated

Mashetani wekundu walitangaza habari hizi kupitia kwenye ukurasa wake.

'Manchester united imethibitisha makubaliano ya kuvunjwa kwa mkataba wa Zlatan Ibrahimovic.' United.

'Kila mtu kwenye klabu angependa kumshukuru Zlatan kwa mchango wake kwenye timu tangia pale alipotua na tunamuombea safari njema kwenye maisha yake ya mbeleni.'


Inatajwa kwamba mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 36 anaweza akajiunga na  La Galaxy inayoshiriki Major league ya marekani, huku Zlatan aliejiunga na Man akitokea PSG mwaka 2016 amebakiza miezi minne tu pekee kwenye mkataba wake.

Akiwa Old Trafford ameweza kujipatia magoli 29 kwenye michezo 53 na kuisaidia United kwenye kunyakua kombe la ligi cup pamoja na kombe la Europa kwenye msimu wa kwanza wa Jose Mourinho.


No comments:

Post a Comment

Pages