UNAJUA KWASABABU GANI BARCELONA INAPENDA KUKUTANA NA ARSENAL, DANI ALVES ATOA UKWELI JUU YA HILI. - BZONE

UNAJUA KWASABABU GANI BARCELONA INAPENDA KUKUTANA NA ARSENAL, DANI ALVES ATOA UKWELI JUU YA HILI.

Share This
Beki kutoka PSG amesema klabu yake ya zamani ilipenda kukutana na washika mitutu kwenye klabu bingwa Ulaya kwasababu......

Mchezaji wa Zamani wa Barcelona Dani Alves amesema klabu kutokea Nou Camp ilipenda sanakukutana na Arsebal kwenye kila mchezo.

Beki huyo alisema walipenda kucheza na washika mitutu kwasababu walikuwa wakiwatawala pale wanapokutana tuu.

Barcelona wamefanikiwa kuweka historia kwenye klabu bingwa Ulaya pale wanapokutana kucheza na vijana wa Arsene Wenger.

Alves alisema "walikuwa na aina ya uchezaji ule ule tuliokuwa nayo sisi na mara nyingine ilitusaidia kuzidisha ufundi kwetu sisi , tulikuwa tunapata sare mara kadhaa (2009/10, 2010/11 na 2015/16 tukiwa tuna songa na matokeo mazuri"

Aliongezea "Ilikuwa ni timu ambayo tulitawala sana. Kila tulipokutana na Arsenal kwenye klabu bingwa Ulaya  tulipata matokeo mazuri yaliotufanya tusonge mbele au kunyakua ubingwa."

Mbio zilianza pale Barca walipoipiga Arsenal mwaka 2006 kwenye fainali zilizofanyika mjini Paris asante kwa Juliano Belleti na Samuel Eto'o waliopiga magoli dakika za mwisho.

Na vile vile Arsenal wakaenda kupoteza ladha kwenye robo fainali msimu wa 2009-2010 pale kijana aliekuwa na umri wa miaka 22 Messi alitengeneza jina na kuanza kuwa kubwa baada ya kuweka magoli manne kambani kwenye dimba la Nou Camp huku Barca wakiongoza magoli 6-3 kwenye aggregate.

Baada ya mwaka Arsenal walikutana na wakatalunya tena lakini mda huu ilikuwa ni hatua ya 16 bora ambapo ushindi ulikuwa ni mwembamba sana lakini kiwango kingine kilicho kizuri kiliwafanya Barca kusonga kwa magoli 4-3 kwenye aggregate

Vijana wa London kaskazini unyonge wao kwa Barca  uliendelea msimu wa 2015/16 ambapo walipangiwa tena kwenye hatua ya 16 bora lakini magoli kutoka kwa Messi, Suarez na Neymar kwenye mizunguko yote ndio yaliowapeleka hatua inayofuata ambapo washika mitutu walikufa kwa magoli 5-1 kwenye aggregate.

Alves tangia haondoke Katalunya amechezea Juventus kwa msimu mmoja tu kalba ya kujiunga na PSG msimu uliopita akiwa huru kwa mkataba wa miaka miwili.

Mbrazili huyu pamoja na Messi ,Andres Iniesta, Gerard Pique, Xavi, Pedro na Sergio Busquests wameweza kuwepo kwenye historia hii. Alves and Arsenal's Francis Coquelin

No comments:

Post a Comment

Pages