RONALDO NA UEFA YAKE,MADRID YAITOA PSG LOS BLANCOS... - BZONE

RONALDO NA UEFA YAKE,MADRID YAITOA PSG LOS BLANCOS...

Share This
Cristiano Ronaldo na Casemiro waiwezesha Madrid kusogea atua inayofuata kwenye mashindano ya klabu bingwa Ulaya.

Kipindi cha kwanza kilikuwa cha kusisimua kaba nikukabe lakini vijana wa Paris ubora ndio waliozidiwa. Karim Benzema alipoteza nafasi kadhaa zilizo bora zaidi na mashuti kadhaa yaliookolewa na Alphonse Areola.

Mbali na hayo yote kipindi cha pili Madrid wakapata mabawa kupitia kichwa cha Ronaldo baada ya kupokea mtungi uliorushwa na Vazquez ndani ya dakika 51 baada ya kupokea through ball toka kwa Marco Ansesio.

PSG hawakutengeneza nafasi za kutosha kabla ya Verrati kupoteza nafasi zao baada ya kumdharau mwamuzi na kupewa kadi ya njano ambayo ilikuwa ya pili kwake yeye, wakati mchezo unaendelea Ansensio alifumua shuti lililoenda kugonga mwamba kabla ya Edinson Cavani kuwawekea PSG goli la kufutia machozi pale mpira ulipomgonga mguuni na kurudi ndani ya nyavu na kufanya kuwa sawa ndani ya dakika zile chache.

Casemiro aliwarudisha Madrid kileleni baada ya mkwaju uliomgonga Areola kwenye dakika ya 80. Isco alikuwa ni mlengwa mkubwa kwenye mchezo wa jana ambapo Mspania huyu alitolewa na kupewa nafasi Ansensio ndani ya dakika chache.

Hutoweza kuamini kuwa Ansensio aliwagharimu Milioni 4 mwaka 2014 pale Madrid walipolidaka dili kutokea Real mallorca.

No comments:

Post a Comment

Pages