Wababe hawa wa Uingereza wamejikuta wapo pamoja baada ya kufanikiwa kusonga kaitika hatua ya robo fainali.
Vijana wa Klopp waliweza kupita hatua ya 16 bora baada ya kuwatoa Porto na watawakaribisha vijana wa Pep Guardiola kwenye mzunguko wa kwanza katika dimba la Anfield.
Kwa upande wa Manchester City waliweza kusonga mbelee baada ya uitembezea kichapo Basel kwa kushinda ugenini 4-0 na kula kichapo cha 2-1 wakiwa nyumbani.
Mabingwa watetezi Real Madrid watakutana tena Juventus ikiwa inarudiwa fainali ya msimu uliopita .
Huku wababe wa Hispania Barcelona kwao inaonekana kama wamepata ganda la ndizi kwa kupata njia ya kujipeleka nusu fainali kilaini..

pale watakapo kutana na Roma.
Lionel Messi ameleta ushawishi mkubwa sana kwenye michuano ya msimu huu kwa kuibamiza Chelsea kwenye mzunguko uliopita.
Bayern Munich wao wataenda kuonana uso kwa uso na wababe wa United ambao ni Sevilla.
Mzunguko wa kwanza utaenda kuanza Aprili 3/4 huku marudiani yakiwa baada ya wiki ambayo iatenda kuwa tarehe 10/11 Aprili.
Mechi zenyewe hizi hapa,
No comments:
Post a Comment