
Awali iliripotiwa kuwa kazi mpya ya Bow Wow ilikuwa Diss kwa Chris Brown, ndio maana ilipewa jina Drunk Off Ciroc.
Shad Moss aka Bow Wow anasema “Mimi na Chris tumepitia mambo mengi kwenye maisha yetu, mambo mabaya tumeweza kuyapita, na kwenye muziki huu na maisha kama kijana utapitia mambo mengi sana, hii ndio ilikuwa maana halisi ya wimbo wangu na sio Chris Brown”.

Bow Wow hajaongea na Chris toka kusambaa kwa taarifa hizi na anasema hana tatizo na Chris Brown, hawezi hata siku moja kuthubuti kumdiss staa huyu.

Bow anasema “Watu waache kutumia hili neno BEEF, sio neno dogo, BEEF ni kile tulichokiona kwa 2 Pac na B.I.G, 50 Cent na Ja Rule, pale ambapo huwezi kuwa na mtu huyo kwenye chumba kimoja, sijawahi kuwa na beef kama hii kwenye maisha yangu”.
No comments:
Post a Comment