
Muimbaji huyo ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa yupo tayari kupigania muziki wake kwa lolote lile na iwapo kuna sehemu ambayo wao kama wasanii wanaenda kinyume ni jambo la kuelekezana.

“Suala si kufungia tu nyimbo, mimi ukinifungia nyimbo hainipunguzii kitu nikienda nje naenda nai-perform ukiwa hutaki sinaondoka tu naenda nchi nyingine, kwa hiyo ni kukaa tuzungumze, tuelekezane lakini tusifanye kama kukomoana, hapana, tufanye katika mazingira ambayo yatasaidia sanaa ikue,” amesema.


Katika hatua nyingine Diamond ametaja kiasi cha fedha alichotumia katika kuandaa stage ambayo ilitumika katika uzinduzi wa albamu yake ya mpya ‘A Boy From Tandale’ uliyofanyika Nairobi nchini Kenya, Diamond amesema stage hiyo iligharimu zaidi ya Tsh. Milioni 150.
No comments:
Post a Comment