"KUNA MDA UNAFIKA UPENDE USIPENDE MWILI LAZIMA UKWAMBIE NI MDA WA KUACHA KUCHEZA MPIRA" MICHAEL CARRICK. - BZONE

"KUNA MDA UNAFIKA UPENDE USIPENDE MWILI LAZIMA UKWAMBIE NI MDA WA KUACHA KUCHEZA MPIRA" MICHAEL CARRICK.

Share This
Michael Carrick amethibitisha kuwa atastaafu soka mwisho wa msimu huu baada ya miaka 12 akiwa Manchester United.

Michael Carrick

Kiungo huyoo mwenye miaka 36 ambae alifanyiwa upasuaji mwanzoni mwa msimu huu na kuwa na matatizo ya mapigo ya moyo yasiyokuwa ya kawaida amefanya maamuzi ya kuacha kucheza soka.

"Kuna mda unafika upende usipende lazima mwili lazima ukwambie hapo ndio mwisho wa kucheza soka," alisema Carrick.
"Ule mda mzuri wote ulikuwa kwangu mimi. Ni kitu lazima ukikubali."



Carrick ambae ameshinda mataji matano ya ligi kuu Uingereza, kombe moja la klabu bingwa Ulaya, kombe moja la FA na makombe matatu ya Ligi, Carrick ameweza kujipatia na kuwa sehemu ya benchi la Mourinho.

"Ni mda wa mipango tu lakini bado tunaendelea kuobgelea iyom ishu kwasasa hakuna kitu chochote kilichowekwa wazi" alisema Carrick.

Kuhusu tatizo la Moyo ambalo lilimkumba septemba Carrick alisema: "Nilikuwa na tatizo kwenye mechi dhidi ya Burton kwenye kipindi cha pili. Nilikuwa na vipimo kadhaa baada ya hapo tatizo limejirudia jumapili nilipokuwa kwenye mazoezi."

'Nimekuwa nikifanya mazoezi kwa juhudi kwa kipindi changu chote na tutaona nini kitachoendelea kwa msimu ujao.'

Carrick alitoa heshima kwa kijana wa United ambae anatumikia sehemu ya kiungo Scott McTominay na akasema kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 amekuwa na uwezo mkubwa sana hasa wa kiakili na amefanikiwa kwa kuwa na mkataba wa mda mrefu pale Old Trafford.




No comments:

Post a Comment

Pages