
Kwa Lampard ni rahisi sana kulitaja jina la Baggio huku likimfanya Ferdinand kujihisi kama anageza kwa jinsi upendo wao walio na kwenye mpira wa kiitaliano kwenye miaka ya 90.

Huku Baggio (Roberto sio Dino) akiwa ni mchezaji pendwa wa Lampard Ferdinand nae akishindwa kujizuia kutompenda aliekuwa mchezaji wa Ac Milan huku wakiwaacha watu kama Frank Rjiikaard na Ruud Gullit.

Tukirudi nyuma na mda pale Parma na Fiorentina zilipokuwa timu zinazo ogopeka barani Ulaya bila kumsahau Batistuta, Weah na Ronaldo walikuwa ni nyota ambao kila mtu alijaribu kuwageza pale walipokuwa mashuleni.
Lampard alijaribu kuelezea kwanini anapenda soka la Serie A. 'kwenye siku hizi za sasa hivi ambapo kuna mitandao ya kijamii kila kitu kipo mkononi unaweza ukaangalia soka la kihispania, soka la Kitaliano, majina haya yapo kwenye muonekano wa kila siku, kwahiyo ilikuwa ni ligi yetu na kulikuwa na mpira wa kimiujiza.'

Lakini kwa pamoja Lampard naFerdinand walimtaja mchezaji pendwa mda wote wa Ac Milan. Baggio mshambuliaji hatari sana ambae alitamba kwenye miaka ya 1990 na 1994 kwenye michuano ya kombe la Dunia na ambae aliweza kuichezea Juventus, Ac Milan na Inter Milan huku Ferdinand akiongezea 'tulizoe kumuita nembo. Alikuwa na skills za kipekee na alikuwa akiishi ndani ya ndoto yake.'
Lampard akaongezea kwa kusema 'Gianfranco Zola alikuwa ni shujaa wangu mwengine.'
"siku zote uwezi kutufananisha sisi na wa Italiano kwasababu wana mbinu za hali ya juu sana."
'Na hapo unaweza ukaona ni maana ya kitu ninacho zungumzia, na kama ukiangalia Uingereza ya nyuma kulikuwa na tofauti kubwa sana ata kimaumbile, nguvu na hata vyakula vyao we muangalie Paolo Di Canio unaweza ukajua nini ninachokisema.'
No comments:
Post a Comment