SIMBA YATUPWA NJE YA MAPINDUZI CUP, UNAZANI NINI KINACHOWASUMBUA WEKUNDU WA MSIMBAZI...!!! - BZONE

SIMBA YATUPWA NJE YA MAPINDUZI CUP, UNAZANI NINI KINACHOWASUMBUA WEKUNDU WA MSIMBAZI...!!!

Share This
Wekundu wa Msimbazi Simba SC wametolewa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar baada ya kuchapwa bao 1-0 na URA ya Uganda ambayo ni timu mwalikwa katika mashindano hayo.
Katika mchezo huo  licha ya Simba kuonesha kandanda safi la kumiliki mpira zaidi katika kipindi cha kwanza ilijikuta ikipigwa bao hilo dakika ya 4 kati ya za nyongeza za kipindi cha kwanza kupitia kwa Bebossi Kalama aliyeichambua safu ya ulinzi ya Simba na kuachia shuti pembeni kabisa mwa lango la Simba.
Kipindi cha pili Simba ilifanya mabadiliko kwa wachezaji watano kwa kuwaingiza Said Ndemla, Mohamed Ibrahim, Yusuph Mlipili, James Kotei na Laudit Mavugo lakini hawakuweza kubadili matokeo, na hadi mwisho wa mchezo, URA bao 1, Simba 0.
Simba inayaaga mashindano hayo ya mwaka huu kutokana na kumaliza katika nafasi ya tatu ya kundi A, ikiwa imeambulia pointi nne pekee katika michezo minne iliyocheza kwenye kundi lake, huku URA wakichukua uongozi wa kundi kwa kufikisha pointi 10 wakifuatiwa na Azam FC nafasi ya pili wenye pointi 9.
Simba ilianza mashindano hayo kwa kutoka sare ya bao 1-1 na Mwenge SC, kisha kuichapa Jamhuri mabao 3-1 katika mchezo wa pili na baadaye kuchezea vichapo viwili mfululizo kimoja kikitoka kwa Azam FC bao 1-0 na kingine cha URA bao 1-0 ilichokipata leo.
URA na Azam wanasubiri matokeo ya mchezo wa mwisho wa kundi B kati ya Yanga na Singida United utakoamua nani acheze na nani katika hatua ya nusu fainali. Kwa mujibu wa utaratibu, mshindi wa kwanza wa kila kundi atacheza na mshindi wa pili kutoka kundi lingine.
Kikosi cha Simba kilichocheza jana ni
Emmanuel Mseja, Nicholas Gyan/Yusuph Mlipili, Asante Kwasi, Juuko Murshid, Erasto Nyoni, Jonas Mkude/James Kotei, Mzamiru Yassin/Laudit Mavugo, Mwinyi Kazimoto/Said Ndemla, Moses Kitandu, John Bocco, Shiza Kichuya/Mohamed Ibrahim.

Je kwa kutoka kwa wekundu wa msimbazi unazanin nini tatizo linalowasumbuwa?

No comments:

Post a Comment

Pages