"TUNAITAJI MIUJIZA KUWAPATA CITY !" LACAZETTE AFUNGUKA JUU YA CITY - BZONE

"TUNAITAJI MIUJIZA KUWAPATA CITY !" LACAZETTE AFUNGUKA JUU YA CITY

Share This
SPORTS: Alexandre Lacazette amekubali kwamaba ata washinde magoli mangapi itakuwa vigumu kuchukua kombe kwa Arsenal msimu huu, alisema alijiunga na klabu ili iweze kwenda klabu bingwa ulaya.

Washika mitutu hao walitoa £52 milioni kuweza kumleta mfaransa huyoo msimu huu  na ameweka mara nane kambani kwenye mashindano yote.

Lakini Arsenal bado wanakaza buti kwenye ligi kuu uingereza wakiwa nyuma ya alama 17 nyuma ya viongozi wa ligi hiyo Manchester City na Lacazette hanaamini kuwa klabu yao hiyoo inaitaji miujiza ili kuweza kumpata Pep Guardiola timu yake.

“Itakuwa ni vigumu sana kupata alama hizi” alisema Mfaransa huyo. “Kikweli tunaitaji muujiza kabisa. City wanatakiwa kupoteza michezo yao yote na tunajua rekodi yao”

Mbali na kuwakatisha tamaaa mashabiki wa Arsenal  maelezo hayo yamelengwa hususani mwezi huu wa Disemba na Lacazette  amesisitiza wanatakiwa sasa hivi kuweka malengo yao ya kucheza klabu bingwa ulaya. Lacazette aliendelea kufunguka na kutaja sababu zilizomtoa Lyon na kumleta kwa wababe wa London kaskazini.

“Ilikuwa ni hali nzuri ya kukutana na kocha na kunifanya niwe hapa nilipokuwepo ni kitu ambacho sikuwahi kutarajia kwenye maisha yangu ya soka tangia nilipokuwa mdogo” alisema
Alimalizia kwa kusema,
“Kila mtu hana kelia yake ya maisha na historia yake”

No comments:

Post a Comment

Pages