Mbali na hiyo msimu huu unaweza ukawa ni wakutushangaza. Hii picha imeweza kuonwa jana usiku Tottenham walivozalisha kiwango kisicho cha kawaida kwa kuwapiga mabingwa watetezi 3-1 wakiwa Wembley.
Wamiliki wa kombe la mabingwa ulaya ambao wameweka historia ya aina yake msimu ulio pita sasa wanapitia kipindi kigumu sana kwa kuweza kulitetea kombe ilo.
Kwenye kundi ilo ilo 2013 Borussia Dortmund wanapitia kipindi kigumu hivo hivo jana walipata aibu kwa kupata sare na Apoel 1-1.
Wajerumani wamekuwa na kampeni mbaya msimu huu wakipata alama mbili tu kwenye mechi na wanaweza wakakosa ata kombe la Europa. Kwa upande wa ndugu zao Bayern Munich ambao wapo kundi B wanatakiwa kufanya kazi ya ziada japo wanashika nafasi ya pili kwenye kundi hao wote wanaangaika kama Real Madrid, Barcelona na Atletico Madrid ambao wote wiki hii hawajapata ushindi.
Barca walibanwa mbavu na Olympiacos kwa sare ya 0-0 na wakiwa kwa mara ya kwanza kutoshinda kwenye atua ya makundi kwa miaka mitano japo watapita kwa hatua inayo fuata. Diego Simeone kwa upande wake yupo nafasi ya tatu na bado hawajashinda huku wakiwa na alama.tatu tuu kwenye kundi lao linalo wajumuisha Azerbaijan.
EBU TUJARIBU KUANGALIA AMBAZO ZINAWEZA ZIKATUSHANGAZA MSIMU HUU.
Paris Saint Germain
Wafaransa hawa wanaonekana kuwa moto safari hii kwa kuwavuta Neymar na kylian Mbappe. Wameshinda mechi zao nne zote ukijumuisha na ile ya Bayern Munich. Lakini hawajawahi fika mbali sana mara nyingi wakiishia robo fainali lakini kwa mwaka huu wanaweza wakatushangaza.
Vipi kuhusu timu za Uingereza?
Ndio, timu za uingereza zimekuwa na.msimu mzuri safari hii kabla ya chelsea kupigwa na Roma haijalishi yanawafanya wanadarajani kupishana alama moja na waitaliano hao hakuna timu ya uingereza iliyoweza kufungwa
Manchester united, City, Liverpool na Tottenham wote wanaongoza makundi yao na hakuna.sababu ya kusema kwanini wasikae katika nafasi izo. Spues na City wameweza kupata michezo migumu lakini wameshinda.
Je kuna klabu nyingine ulaya?
Roma wanaonekana wapo vizuri kwenye C na wamezalisha kiwango kizuri dhidi ya Chelsea
mbali na hiyo japo hawafanyi vizuri kwenye Seria A inaonekana wapejipanga kwenye ligi ya mabingwa ulaya. Atuwezi kuisahau Juventus pia hawafanyi kama wanavyo fanya Roma wakiwa nafasi ya pili wakipishana na Barcelona kwa alama mbili wakiwa wameshinda michezo miwili.
No comments:
Post a Comment