Ernasto Valverde kwa upande wake unaweza ukaongeza baadhi ya alama nakufikisha alama saba kileleni kawa wakiwapiga Leganes leo Jumamosi.
Lionel Messi, Luis Suarez na Gerald Pique wote walionekana mazoezini kwenye dimba la Sant Joan Despi.
Barcelona hawajapoteza mchezo wao wa ligi kati ya yote waliocheza na wameshinda michezo 10 kati ya michezo 11 waliocheza, mbali na hiyo wamekuwa na mwanzo mzuri wa msimu huku kocha Valvarde amewaonya wanaoleta lawama kwenye kikosi chake.
Leganes wapo nafasi ya 9 kwenye La liga na Valverde wanaamini kwamba watapata heshima kupitia mchezo huo.
Alisema ‘Kwa kocha yeyote yule kwenye mchezo kama huu inabdi achukue tahadhari kubwa sana hasa kwa viwanja vya ugenini.
Beki Thomas Vermaelen ambae alionekana pia mazoezini anaweza akacheza mchezo wake wa kwanza wa ligi pamoja na Javier Macherano anaweza asiwepo kwa kusumbuliwa na misuli ya paja.
No comments:
Post a Comment