
Manara amesema hayo mapema baada ya timu yake kulazimishwa sare ya goli 1-1 dhidi ya klabu ya Lipuli FC kutoka mkoani Iringa.

'chukueni hatua kubwa isiishie tu kumsimamisha' amesema Haji Manara mapema baada ya mchezo kumalizika huku akimlaumu Mwamuzi wa mchezo wa leo dhidi ya Lipuli FC.
“Maana adhabu kubwa utasikia amesimamishwa hata malizia mzunguko huu, pigeni kifungo au kufuta waamuzi wa hovyo, hakuna kitu kinachoumiza mpira wa Tanzania kama uamuzi mbovu. Nasema matokeo yake naonekana kama mkorofi, mlalamishi au nawaonea waamuzi lakini macho yote yanaona na mmeshuhudia pale kilichotokea, tumenyimwa penati ya wazi lakini sitaki kulalamika, nikilalamika ntaonekana nalalamikia waamuzi, chukueni hatua kama mkiridhika waamuzi hawachezeshi vizuri.”
Haji Manara mwezi uliopita alibeba Tv mbele ya Waandishi wa Habari akilalamikia Mwamuzi wa mchezo wao dhidi ya Yanga kuwa amewanyima penati na kuahidi kupeleka suala hilo serikalini kupitia wizara ya Habari na Michezo.
No comments:
Post a Comment