Ronaldo amefanikiwa kupata mtoto huyo kupitia kwa mpenzi wake ambaye ni mwanamitindo wa nchini Hispania, Georgina Rodriguez.
Kupitia mtandao wa Instagram, mchezaji huyo ameandika jina la mtoto huyo ni Alana Martina.
Watoto wengine wa mchezaji huyo ni Cristiano Ronaldo Jr mwenye miaka saba na mapacha wake aliwapata mwaka huu Eva Maria na Mateo ambao mama yao bado hajafahamika.
No comments:
Post a Comment