Kwenye mchakamchaka wa Ligi ya Europa inaonekana washika bunduki wamesafiri kwenye uwanja wa Majko Mitic almaarufu kama Marakana, ambapo mashabiki zaidi ya 50000 wataingia uwanjani kuona timu yao ikimenyana huku kukiwaa na mabango ya kutisha.
Kama wachezaji wa Asernal hawajui kama watakutana na nini kwenye hatua hii, basi wakati wanaingia uwanjani watatembea kwenye handaki chini lenye urefu mkubwa na uwanja ukiwa kama bakuli.
Itachukua kama dakika kwenye chumba cha kubadilishia nguo kabla ya kuingia uwanjani wakiwa wanatembea kwenye handaki linalotisha likiwa na michoro ya ajabu kwenye kuta.
michezo mikubwa hasa kwenye mji wao 'derby' wakicheza na Partizan Belgrade namba kubwa ya polisi wenye silaha huwepo.
Makelele ya mashabiki zaidi ya 55000 kwenye viti watasikika huku timu zikicheza, baruti za moto zenye makelele zitakua zikisikika wakati ukiwa unasogelea uwanjani.
Wamekuwa na mafanikio nje ya nchi yao pia kwa kushinda kombe la ulaya mwaka 1991 kwa mikwaju ya penati zidi ya Marseille 0-0 Bari , Italy. Pia ishawahi kuwa na majina makubwa kama Sinisa Mihajilovic, Rober Prosinecki, Vladimir Jugovic na Dejan Savicevic. Academy yao iliweza kuwazalisha watu kama Nemanja Vidic na Dejan stankovic aliechezea inter
No comments:
Post a Comment