mshambuliaji huyo mwenye magoli saba kwenye michezo nane tangia ajiunge na wababe hao wa darajani akitokea Real Madrid alitolewa nje kwenye mchezo wa Chelsea waliopigwa 1-0 na Manchester city baada ya dakika kumi tu.
Kocha Antonio Conte baada ya mchezo aliweza kufunguka juu ya mshambuliaji huyo juu ya kumtoa haraka na kusema Morata alikuwa kwenye tahadhari kubwa, Lakini mshambuliaji huyu alienda jijini Madrid kuangaliwa na jana jumatatu shirikisho la mpira uhispania likasema kwamba mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anasumbuliwa na misuli ya paja ambayo ipo kwenye hawamu ya pili.
No comments:
Post a Comment