POGBA AMEUMIA KIPINDI TUNACHOMUHITAJI ZAIDI-MIKHITARYAN - BZONE

POGBA AMEUMIA KIPINDI TUNACHOMUHITAJI ZAIDI-MIKHITARYAN

Share This
Paul Pogba, Manchester United, Henrikh Mkhitaryan, English Premier LeagueNA ABDUL KHALID,
SPORTS: Winga  machachari wa klabu ya Manchester united Henrikh Mkhitaryan amesema kwamba kuumia kwa kiungo mwenzake Paul pogba ambaye atakuwanje ya dimba kwa kipindi kirefu kidogo kutafanya maisha ndani ya timu hiyo kuwa magumu kutokana na mchango uliokuwa ukitolewa na kiungo huyo raia wa ufaransa.

Pogba ambae anasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja anatazamiwa kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na daktari wa miamba hiyo ya Old  Trafford.

Mikhitaryan anakubali kuwa wamemkosa mtu muhimu sana katika timu yao iliyo kwenye mbio za kutwaa taji la ligi kuu ya Uingereza msimu huu na kusema kuwa bado kikosi chao bado kina nafasi ya kuendelea kufanya vizuri msimu huu.

"Itakuwani vigumu sana kwetu bila Paul, kwa sababu yeye ni mchezaji wa kiwango cha juu, lakini kocha anajua nin jinsi gani atafanya ili kupunguza ukubwa wa pengo lake hadi atakaporejea tena kikosini" Mikhitaryan akimzungumzia Pogba.

No comments:

Post a Comment

Pages