HONGERENI YANGA MMETUONESHA KUWA WEMA HAUOZI..!! - BZONE

HONGERENI YANGA MMETUONESHA KUWA WEMA HAUOZI..!!

Share This
NA ABDUL KHALID,
SPORTS: Nilitamani nikae kimya lakini naona kama sijitendei haki kama nisipolizungumzia hili na kupata ufafanuzi, 

1. Kwa upande wangu naona wana yanga hawakukosea kwenda kumpa pole mwenyekiti wao manji kwani ni mtu  muhimu sana kwa yanga tunayoijua na siasa zake.
Manji ni aliikuta timu iyoo kwenye mgogoro wa yanga kampuni dhidi yanga asili lakini akatumia ushawishi wake kuinusuru timu isigawanyike kama ilivyowahi kutokea na kupelekea kuundwa kwa Pan afrikani mwaka 1975/76 

2.Suala la kuwa mwenyekiti ni la uongozi na mara kadhaa Manji amekuwa na nia hiyo lakini kama kwa mtu makini unatengeneza vipi uwanja mahala unapopingwa kwa hoja dhaifu mradi tu mtu anajua akienda mahakamani kuweka zuio basi anasimamisha kila kitu, 
Manji ni mfanya biashara makini na  anafahamu fkuwa akiwekeza atapata nini na klabu itapata nini, nikulize kitu kimoja msomaji wa safu hii hivi Raisi wa Madrid au Barcelona alijenga uwanja kwa pesa zake mfukoni? jibu hilo baki nalo ila kwa leo ningeomba unijibu hili., kwa kigezo cha manji kuwa na pesa  basi ni lazzima aifanyie yanga kila kitu? 

3. Manji ni mfadhili kwa mapenzi yake tu anatoa mishahara analipia usafiri na usajili na gharama chungu nzima ndani mwaklabu  hiyo kongwe hapa jijini pia ameleta pendekezo la kuikodi btimu iyo.
Na sio klabu ieleweke! ni timu ya mpira waliikimbilia mahakamani na badala yake hawakuja na hoja mbadala zenye mashiko, hata kama ni malaika ataamua kukaa pembeni awaangalie kina Juma magoma, mzee Akilimali wanavyoiumbisha Yanga.

4. Manji anajtolea na hata kwa cheo chake kama vmwenyekiti  kwa muundo huu wa katiba ya yanga hata aje Sheikh Makhtoom bado wakongwe hao hawatapiga hatua kimaendeleo.

5. Uongozi wa yanga wao wenyewe wanatambua umuhimu na mchango wa Manji katika kikosi cha timu hiyo yao na hiyo ndio sababu kubwa mpaka leo hii hawajibu barua ya bosi huyo aliyetaka kujiuzulu wadhifa wa uenyekiti.

6.Licha ya hivyo bado kuna kazi kubwa ya kuendelea kumshawishi kuendelea kuwa nae karibu hasa baada ya kumtoa kama mdhamini mkuu mbele ya jezi ya timu kwani hilo lilikuwa jambo kubwa la Manji ambalo alikuwa akijivunia.

No comments:

Post a Comment

Pages