Mpaka sasa Bodi ya usajili ya Manchester United imekamilisha usajili wa beki Victor Lindelof kutoka Benfica kwa ada ya Paundi Milioni 31 huku usajili wa nyota wengine anaowataka Mourinho akiwemo Alvaro Morata wa Real Madrid, Ivan Perisic kutoka Inter Millan pamoja na kiungo Nemanja Matic ukionekana kusua sua jambo ambalo kocha huyo hajafurahishwa naloKwa Mujibu wa Gazeti la “The Sun” la nchini Uingereza Jose Mourinho amekasirishwa na Uongozi wa United kushindwa kukamilisha usajili mapema kutokana na mipango ya kocha huyo kutaka wachezaji wote wanaosajiliwa majira haya wafanye mazoezi ya pamoja nchini Marekani katika maandalizi ya Msimu ujao wa ligi huku zikiwa zimesalia siku nane Wachezaji waripoti kambini.

Manchester United inahisishwa na wachezaji wengi kutoka ligi mbalimbali barani ulaya ili kukijenga kikosi chao kilichotingwa katika Michuano ya UEFA Champions baada ya kunyakua Ubingwa wa EUROPA.
No comments:
Post a Comment