CHIN BEES AIBUKA NA MENGINE KUHUSU ‘UP IN THE AIR’ YA ROSA REE - BZONE

CHIN BEES AIBUKA NA MENGINE KUHUSU ‘UP IN THE AIR’ YA ROSA REE

Share This


ENTERTAIMENT: Rapa Chin Bees kutoka Wanene Entertainment anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Pepeta’ amerusha tuhuma nyingine kuhusu wimbo wa ‘Up In The Air’ wa rapa wa kike Rosa Ree anayefanya kazi chini The Industry.

Kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio Chin Bees ameonesha kutoridhika na kutumika kwa wazo lake la Chorus katika wimbo wa ‘Up In The Air’ bila kupewa taarifa, wimbo ambao unatajwa kuwa kati ya nyimbo ambazo zimefanya vizuri mpaka sasa tangu kutoka kwake mwazoni mwa mwaka huu.

Hata hivyo Chin alishasema kuwa mbali na kuwa ameshiriki kuandika nyimbo kadhaa kubwa za Navy Kenzo ikiwemo ‘Kamatia Chini’, kutopewa Credit za ushiriki wake katika baadhi ya nyimbo ni moja ya sababu zilizompelekea kutokuwepo The Industry.

No comments:

Post a Comment

Pages