STARS KUWAVAA LESOTHO LEO - BZONE

STARS KUWAVAA LESOTHO LEO

Share This
SPORTS: Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajiwa kushuka dimbani leo kutupa karata yake ya mwisho dhidi ya Lesotho kwa ajili ya kutafuta nafasi ya mshindi wa tatu ya michuano ya COSAFA . Mchezo huo utakaochezwa uwanja wa Moruleng mjini Rusternburg, Afrika Kusini majira ya saa 2:oo usiku utakuwa wenye mvuto kiaina kwani hii itakuwa ni mara ya pili Stars kuvaana na Lesotho kwa mwaka huu ambapo mchezo wa kwanza ulikuwa ni wa kufuzu michuano ya AFCON uliopigwa hapa nchini ambapo tuliona timu zote mbili zikitoshana nguvu kwa sare ya goli 1-1 .
Hatua hiyo ya Tanzania kukutana na Lesotho imekuja baada ya timu zote mbili kufungwa katika hatua ya nusu fainali ambapo Lesotho walichapwa 4-3 na Zimbabwe huku Taifa Stars ikiambulia kichapo cha 4-2 dhidi ya Zambia.
Mchezo wa fainali ya michuano hiyo kati ya Zambia na Zimbabwe utachezwa siku ya Jumapili ya tarehe 9 julai majira ya saa 10:00 jioni.

No comments:

Post a Comment

Pages