SIFANYI MZIKI KIUSHINDANI MIMI-ALI KIBA - BZONE

SIFANYI MZIKI KIUSHINDANI MIMI-ALI KIBA

Share This


ENTERTAIMENT: Msanii wa Bongo Fleva, Ali kiba amewachana wale wote wasanii ambao wanataka kushindana nae kwa kusema kuwa yeye katika muziki wake hakuna mtu wa kushindana  naye kwani hafanyi muziki wa kushindana na kama watafanya hivyo basi atawaacha washindane .  Akifunguka kwenye mahojiano yake na kituo cha Capital FM cha nchini Kenya, Ali Kiba amesema katika maisha yake ya muziki hataki kuona mtu yoyote anamtoa katika njia yake, ndiyo maana watu ambao wanakuwa wakiongea ongea sana juu yake yeye na muziki wake hawapi nafasi, kwani anaamini akiwapa nafasi wanaweza kumtoa kwenye mambo ambayo yeye amekusudia kuyafanya hasa zaidi katika muziki wake ndiyo maana hafanyi muziki kwa kushindana.

“Kila binadamu yupo na tabia yake  kuna wengine wanafanya vitu wanajua wanakosea wanafanya makusudi na kuna wengine wanaongea lakini hawajui kama wanakosea so mimi kama mwanamuziki sitaki kuwasikiliza hao  kwa sababu nina Target yangu ninavitu vya kufuatilia  sitaki  hata mtu yeyote aniingilie kwenye Target yangu kwahiyo kama utawafuatilia utapotea sifanyi muziki kwa kushindana kama hao watafanya muziki kwa kushindana nitawaacha washindane  “ alisema Ali Kiba kwenye mahojiano yake na Capital Radio ya Kenya .
Ali Kiba ambaye yupo nchini Kenya kurekodi kipindi cha Coke Studio Africa Season 5 ameahidi kuachia ngoma muda si mrefu hivyo amewataka mashabiki wasimpe presha ya kumfosi kutoa ngoma kwani muziki anaoufanya ni kwa ajili yao na kwake pia.

No comments:

Post a Comment

Pages