SCHNEIDERLIN ATUA BONGO NA MKE WAKE KWAJILI YA BATA - BZONE

SCHNEIDERLIN ATUA BONGO NA MKE WAKE KWAJILI YA BATA

Share This
SPORTS: Baada ya David Beckham, Mamadou Sakho, Victor Wanyama na Christian Eriksen kutua nchini kwaajili ya kutalii, Jumanne hii mchezaji wa Everton, Morgan Schneiderlin ametua nchini kwaajili ya honeymoon na mke wake. Kiungo huyo ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, atakuwa mmoja kati ya wachezaji wa Everton ambao watatua nchini Julai 13 kwaajili ya mchezo wao wa kirafiki dhidi mshindi wa SportPesa Super Cup, Gor Mahia.
Schneiderlin kupitia ukurasa wake wa Instagram amepost picha akiwa mbugani na kuandika “First day of our honey moon ❤ #tanzania #safari 😍😍!”
Schneiderlin alifunga ndoa Juni 12 na mpenzi wake huyo wa muda mrefu aitwaye Camille Sold. Angalia picha.

No comments:

Post a Comment

Pages