WCB WASAFI KUTAMBULISHA MSANII MPYA LEO - BZONE

WCB WASAFI KUTAMBULISHA MSANII MPYA LEO

Share This
ENTERTAIMENT: WCB Wasafi pamoja na ukubwa ambao wanao, lakini bado ni lebo ambayo inaendelea kuonyesha nia ya kutimiza ndoto za vijana wengi wa mitaani wenye vipaji.
Walianza na Harmonize ambaye hakuna aliyemtambua kabla, ila leo hii ni mmoja kati ya wasanii wakubwa barani Africa, wakafuata Rayvanny ambaye leo hii kila jicho la mpenzi wa muziki mzuri barani Africa linamtazama yeye, hawakusita pia kwa Rich Mavoko ambaye ni mkongwe aliyeonekana kuyumba kimuziki lakini leo hii ni mkali aliyesimama vyema kwenye A List ya Wasanii Tanzania, na pia Leo WCB wanatarajia kutambulisha kichwa kipya kwa mara nyingine.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Diamond Platnumz ametusanua kuwa Leo kwenye Leo Tena yaClouds FM wataweza kukitambulisha kichwa kipya kwenye ramani ya muziki.
Diamond kupitia page yake ya instagram aliandika kuwa “Panapo majaaliwa siku ya jumatatu kesho, ntakuwepo kwenye LEO TENA ya Clouds fm na familia nzima ya @Wcb_wasafi tukimtambulisha Kijana mwenzetu Mwingine Mpya toka Mtaani, ndani ya @Wcb_Wasafi….. Sisi ni vijana ambao tumekulia kwenye umaskini na bado tupo kwenye kupambana namna ya kujikwamua kwenye umasikini… na ndiomaana tunajitahidi kadri ya uwezo wetu kila tukiona kijana yoyote mwenye nia na kipaji kumsaidia kwa kadri ya uwezo wetu, ili nae aweze kutambulisha kazi zake, na Pengine Mwenyez Mungu akimjaalia nae awe mkombozi kwenye Familia yake….Sio jambo Rahisi ni gumu, lakini kwa Sapoti yenu naamini tunaweza lifanikisha…Siku zote naomba mkumbuke WCB_Wasafi sio ya Diamond, ni ya vijana wote wapambanaji…na ndiomaana kila siku nawaomba Muendelee kuniombea na Kunisapoti, kwani Sapoti yenu ndio itayo nifanya hata kesho niweze kukuchukua wewe ama ndugu yako ili aje kukitambulisha kipaji chake na Mwenyez Mungu akijaalia kufikia Malengo…… USIKOSE kusikiliza Leo tena ya @Cloudsfmtz saa nne Asubuhi…Shukran🙏

No comments:

Post a Comment

Pages