NIPO MWANZA ILI KUONGEZA BAO - BZONE

NIPO MWANZA ILI KUONGEZA BAO

Share This
SPORTS: WINGA wa Yanga, Simon Happygod Msuva amesema anakwenda Mwanza kuongeza mabao ili atimize malengo yake ya kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mara ya pili ndani ya misimu mitatu.
Yanga wanatarajiwa kuwa wageni wa Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza Leo katika mchezo wa kufunga pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

 Msuva alisema kwamba baada ya kuukosa mchezo uliopita kutokana na kuwa majeruhi anataka kumaliza msimu vizuri.
“Ni mchezo ambao tunakwenda kumalizia msimu, mchezo ambao tunatakiwa kuutumia kuwaaga vizuri mashabiki wetu, lakini pia kwa mtu kama mimi kuutumia pia kuongeza mabao ili nifanikishe azma yangu ya kuwa mfungaji bora,”alisema. 

Msuva anaongoza kwa mabao yake 14 Ligi Kuu, akifuatiwa na Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting mwenye mabao 13 na Mbaraka Yussuf wa Kagera Sugar mabao 12.
Na akifanikiwa kuchukua tena na msimu huu, Msuva ataweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu mara mbili, baada ya awali kubeba tuzo hiyo msimu wa 2014 – 2015.
Na atakuwa mchezaji wa pili tu kuchukua tuzo hiyo mara mbili tangu mfumo mpya wa Ligi Kuu kuchezwa ndani ya miaka miwili kuanzia msimu wa 2007 – 2008, mwingine akiwa ni Mrundi, Amissi Tambwe.
Tambwe ambaye anashikilia tuzo hiyo kwa sasa baada ya kuitwaa msimu uliopita akiwa Yanga, ndiye mfungaji bora pia wa msimu wa 2013 – 2014 akiwa Simba.  


WAFUNGAJI BORA LIGI KUU TANGU 2007- 2008
Msimu           Mchezaji                  Timu             Mabao
2015 – 2016: Amissi Tambwe  Yanga SC 21
2014 – 2015: Simon Msuva Yanga SC 17
2013 – 2014: Amissi Tambwe  Simba SC 19
2012 – 2013: Kipre Tchetche  Azam FC 17
2011 – 2012: John Bocco  Azam FC 19
2010 – 2011: Mrisho Ngassa  Azam FC 18
2009 – 2010:  Mussa Mgosi  Simba SC 18
2008 – 2009:  Boniphace Ambani  Yanga SC 18
2007 – 2008:  Michael Katende  Kagera Sugar  11

No comments:

Post a Comment

Pages