HII NDIO AHADI YA ZARI KWA WATOTO WA IVAN - BZONE

HII NDIO AHADI YA ZARI KWA WATOTO WA IVAN

Share This
MIX: Zari Hassan amezungumza kwa mara ya kwanza tangu mume wake wa zamani, Ivan Semwanga afariki dunia. Katika misa ya mazishi iliyofanyika kwenye kanisa la Namirembe mijini Kampala, Uganda Jumatatu hii, Zari alionekana akiwa ametulia na akizungumza na wanae.
Alipoitwa kuzungumza madhabahuni, watu waliohudhuria walijianda kumsikiliza atakachosema.
“Sitomhuzunikia Ivan,” alisema. “Nitasherehekea maisha yake. Muda mrefu, tulitengana kwasababu ya tofauti ambazo sote tulizijua. Nilisonga mbele na maisha yangu, lakini si Ivan. Ivan alijua kile nilichoweza kufanya. Alijua kile nilichoweza kufanya na kile nisichoweza. Alijua kuwa ningewaangalia vijana vyema na aliniamini. Kwa hali hiyo, naahidi ntawaangalia vijana hadi nitakapoungana naye.”
Ivan anatarajiwa kuzikwa kesho ambapo Diamond aliyezaa na Zari watoto wawili naye aliahidi atahudhuria.

No comments:

Post a Comment

Pages