HUDDERSFIELD TOWN FC YAPANDISHWA DARAJA LIGI KUU UINGEREZA - BZONE

HUDDERSFIELD TOWN FC YAPANDISHWA DARAJA LIGI KUU UINGEREZA

Share This
Photo published for Reading vs Town: Your quick-fire talking points from WembleySPORTS: Klabu ya Huddersfield Town imepandishwa daraja kucheza Ligi ya Premia kwa mara ya kwanza baada ya kulaza Reading 4-3 kupitia mikwaju ya penalti uwanjani Wembley Jumatatu.
Baada ya kutoka sare 0-0 dakika 120, Town walitakiwa kupiga mikwaju kwa mara ya pili na walikuwa na bahati tena baada ya kulaza pia Sheffield Wednesday kwa mikwaju ya penalti hatua ya nusufainali.
Christopher Schindler aliwashindia Town baada ya mkwaju wa Liam Moore kupaa angani nao mpira wa Jordan Obita ukaokolewa na kipa Danny Ward.
Klabu hiyo ya Yorkshire Magharibi haijacheza soka ya ligi kuu tangu 1972.
Reading, waliomaliza alama nne na nafasi mbili juu ya Town waliokuwa nafasi ya tano katika ligi ya Championship sasa wameshindwa katika fainali ya muondoano ya kufuzu kwa EPL baada ya ligi kwa mara ya nne.

No comments:

Post a Comment

Pages