
Mwanamuziki huyo wa muziki wa Pop aliongeza utajiri wake kutoka pauni milioni 85 hadi pauni milioni 125 ikimaanisha ndiye mwanamuziki tajiri zaidi wa kike katika gazeti hilo linaloangaiza utajiri wa wanamuziki kila mwaka.
Hatahivyo ameshikilia nafasi ya 19 pamoja na mwanamuziki mwengine wa kiume katika oroadha ya wanamuziki matajiri nchini Uingereza ambayo imetawaliwa na wanamuziki wa kiume.
Wanafuatwa na West End Mogul Lord Lioyd Webber, U2, Sir Elton John, Sir Mick Jagger na mpiga bendi mwenza wa Rolling stones Keith Richards.Adele anashikilia nafasi ya 19 akiwa na pauni milioni 125 pamoja na mpiga gita wa Queen Brian May.
Kuongezeka kwa utajiri wake kunadaiwa kutokana na ziara 122 za ulimwenguni ambazo zilimpatia kitita cha pauni milioni 138 mbali na ufanisi wake wa albamu yake ya tatu 25 ambayo iliuza kopi 2.4 duniani 2016.
Msanii huyo atahudhuria halfa ya muziki iliouza katika uwanja wa Wembley lakini ametoa ishara kwamba hatofanya ziara nyngine, hatua ambayo huenda ikamzuia kutajirika zaidi.

No comments:
Post a Comment