Timu ya Serengeti Boys yaalikwa bungeni - BZONE

Timu ya Serengeti Boys yaalikwa bungeni

Share This
SPORTS: Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys leo watakuwa bungeni, Dodoma kwa mwaliko maalumu wa Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) inachukua nafasi hii kuishukuru ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuialika timu ya taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ya Tanzania maarufu kwa jina la Serengeti Boys.
Timu hiyo ambayo tayari imepata barua ya pongezi kutoka kwa spika wa bunge, imeitikia wito wakufika bungeni na kupata nafasi ya kuingia bungeni katika vikao vya bunge vinavyoendelea Dodoma.
Serengeti Boys ni timu ya mpira wa miguu ya wavulana ambayo imefuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika nchini Gabon kuanzia Mei 21, mwaka huu.
Timu hiyo imeondoka na wajumbe nane(8) wakiongozwa na Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania Jamal Emil Malinzi wajumbe wengine ni kama wafuatavyo:
1. Ayoub Nyenzi – Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Mpira wa Miguu kwa vijana kutoka Kamati ya Utendaji TFF
2. Mulamu Ng’ambi – Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA)
3. Salum Madadi- Mkurugenzi wa Ufundi TFF
4. Alfred Lucas – Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF
5. Kim Poulsen – Mshauri wa Ufundi wa Soka la Vijana
6. Mwarami Mohammed – Kocha wa makipa wa Serengeti Boys
7. Edward Venance – Mtunza Vifaa wa Serengeti Boys

No comments:

Post a Comment

Pages