JASON DERULO ACHUKIZWA NA KITENDO HIKI CHA SHIRIKA LA NDEGE LA AMERICAN AIRLINES, AFUNGUKA MAZITO - BZONE

JASON DERULO ACHUKIZWA NA KITENDO HIKI CHA SHIRIKA LA NDEGE LA AMERICAN AIRLINES, AFUNGUKA MAZITO

Share This
ENTERTAIMENT: Muimbaji wa muziki wa RnB wa Marekani, Jason Derulo afunguka mazito na kulishutumu moja kwa moja shirika la ndege la ‘American Airlines’ kwa ubaguzi wa rangi. Derulo adai kutukanwa na wafanyakazi kadhaa wa shirika hilo baada ya kutokea malumbano kuhusiana na malipo ya mizigo yake.
Amedai kuwa baada ya kumgundua kuwa ni mtu maarufu walibadilisha lugha. Derulo ameiambia tovuti ya PEOPLE kuwa, alikuwa akisafiri kutoka Miami kwenda Los Angeles na anasema baada ya kuonekana wangechukua muda mwingi wa ukaguzi, waliamua kumwacha mtu mmoja ashughulikie mizigo wao wakatangulia.
Kwa mujibu wa chanzo kutoka kwenye kampuni ya Airlines, kimedai kuwa mabegi matatu pekee ndiyo hukaguliwa bure lakini rafiki wa Derulo alikuwa na mabegi 19 hivyo akatozwa gharama za ziada. Muimbaji huyo anasema alikuwa kwenye ndege ndipo alipopigiwa simu na rafiki yake aliyemweleza kuwa American Airlines walitaka kumtoza $4,000 kwaajili ya mabegi hayo.
Kwenye maelezo yake kwa PEOPLE, American Airlines imesema ndege hiyo, Flight 275 ilirudi kwenye geti la kuondokea na Derulo akashuka kwaajili ya kushughulikia mabegi yake. Derulo anadai wakati yeye na rafiki zake wakishuka kwenye ndege, rubani alitoka na kuanza kuwatukana.
“And that was really upsetting to me because I felt like he was trying to make it seem like we were delinquents, and he was kicking us off the plane, when it was us that asked to get off the plane. I was like, ‘Listen, sir, you’re not going to talk down to me; I’m not your son. Don’t talk to me in that tone of voice,” amesema Derulo.
Derulo amesema baada ya kushuka kwenye ndege, yeye na washkaji zake walikutana na polisi 15 na muda huo mfanyakazi mwingine wa shirika hilo akaanza kuwatukana.
“As you can imagine, I’m surrounded by 15 police officers, I’m not going to curse back because I know what’s going to happen,” anasema. “So I pick up my phone, and I go live on my Instagram.”
“So I go live, and I start to hear whispers happening, and as soon as they find out who I am, everything changes. Every single person becomes somebody else, and all of a sudden, we’re not in trouble anymore.”
Picha hailikuishia hapo, mkali huyo akatumia pia ukurasa wake Instagram kutoa malalamiko yake..

No comments:

Post a Comment

Pages