ENTERTAIMENT Maamuzi ya Trump ya kuzuia wahamiaji kutoka katika mataifa ya kiislamu kuingia nchini Marekani, yameanza kuwatafuna watu mashuhuri nchini humo.
Kama mwezi uliopita baada ya Trump kutangaza kupinga kwa waislamu kutoka mataifa ya Iraq, Somalia, Iran na zingine kibao, Baby Mama wa Kanye West, Kim Kardashian amekutana na msala wa kusachiwa ndege yake pindi alipotua baada ya kutoka visiwa vya Costa Rica.
Baadhi ya mashabiki wamefunguka na kusema kwamba Custom Office hao ambao walikuja kuisachi ndege ya Kim, imekuja pindi Kim alipotweet kuhusiana na kupinga ule uamuzi wa Donald Trump kwa kuposti picha ambayo inaonyesha takwimu ya mauaji nchini Marekani ambayo yaliwahi kutokea.
No comments:
Post a Comment