HII HAPA ORODHA YA WAIGIZAJI WA FILAMU ZA KIHINDI WALIOTIKISA ENZI HIZO - BZONE

HII HAPA ORODHA YA WAIGIZAJI WA FILAMU ZA KIHINDI WALIOTIKISA ENZI HIZO

Share This
Pamoja na kwamba uigizaji wa filamu za Kihindi unaendelea hadi hivi sasa, lakini kamwe ubora na umahiri wake wa waigizaji hauwezi kufikia wa enzi hizo wa miaka ya 1960 hadi 1990.
Waigizaji wa filamu za Kihindi wa enzi hizo walikuwa wakionesha umahiri wa hali ya juu ambao hadi hivi leo ukizitazama utaona kuwa bado zinavutia na zina hisia kali kwa wapenzi wa sinema hizo.
Vitu vilivyowasukuma wapenzi kuangalia filamu hizo ni namna ya ubunifu uliokuwa ukioneshwa na waigizaji hao, uimbaji na uchezaji, namna ya uigizaji wa kikatili uliokuwa ukioneshwa na mapenzi yaliyokuwa yakioneshwa kutoka kwa washiriki wa picha hizo.
Licha ya kwamba filamu hizo za Kihindi za wakati huo zilikuwa ni za kuigiza, lakini matukio yaliyokuwa yakioneshwa kama ya mapenzi, visasi, ubabe yalionekana kuwa kama ni ya kweli hali iliyosababisha picha hizo kupata wapenzi wengi duniani kote hususani katika bara letu la Afrika.
Miongoni mwa filamu hizo za Kihindi ambazo hadi leo hii bado zinakumbukwa na wapenzi wa picha hizo ni SholayAndhaa KaanoonKaalia, DonShanCoolieNaseebSuhaagAmar Akbar AnthonyNargin, Yaadon Ki BaratSuhaag, DostJugnuBobby, Kabhie Kabhie, Mugaddar Ka Sikandar,
Nyingine ni DharmatmaInsaniyatGeraftaarPukarParvanshHum Kisise Kum Nahin,Kartavya, Fifty FiftyGangaa Jamumaa na Desh Premee.
Wafuatao ni miongoni mwa waigizaji wa filamu za Kihindi waliovuma na kutamba katika miaka ya 1960 hadi 1990.
1.AMITABH BACHCHAN
Bachchan ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 74, ni miongoni mwa waigizaji wa filamu za Kihindi ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na kuigiza akiwa katika sura tofauti zikiwemo uharamia, askari, mzee wa busara na vichekesho.

Pamoja na umahiri mkubwa aliokuwa nao wa kumudu kuigiza akiwa katika sura zote hizo, pia alikuwa fundi mno katika kuimba na kucheza miziki ya Kihindi.
Mkongwe huyo alianza kujulikana katika tasnia hii ya filamu za Kihindi miaka ya 1970 alipoigiza filamu mbili, Zanjeer na Deewaar, ambazo zilimpatia umaarufu mkubwa. Mwaka 1975, Bachchan aliigiza filamu nyingine akiwa na Dharmendra Sholay ambayo ilizidi kumjengea jina ambapo sasa alizidi kupata uzoefu.
Sholay hadi hivi leo bado ni gumzo kwa wapenzi wa filamu za Kihindi. Katika filamu hiyo, Bachachan aliigiza akiwa na waigizaji wengine mahiri kama Amjad Khan, Hema Malini, Jaya Bhaduri, Sanjeev Kumar, Asran na Mac Mohan kama Sambha.
Sholay ni miongoni mwa filamu bora ya Kihindi kuwahi kutokea na inashika nafasi ya kwanza kati ya sinema 10 bora kwa wakati wote. Mwaka 2005, ilipata tuzo ya sinema bora kwa miaka 50 iliyopita.
Mbali na Sholay ambayo ilimjengea jina kubwa, pia aliendelea kuigiza filamu nyingine ambazo nazo zilivuma ikiwemo Kaalia, Andhaa Kaanoon, Don, Desh Premee, Coolie, Naseeb, Suhaag, Insaniyat na Mr Natwarlal. Kuanzia miaka ya 1870 hadi mwaka jana 2016, Bachchan amefanikiwa kuigiza zaidi ya filamu 190.
2. DHARMENDRA
Dharmendra ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 81, naye kama alivyo Bachchan ni miongoni mwa waigizaji wa filamu za Kihindi ambao walijipatia umaarufu mkubwa huku akianza kuvuma kabla ya Bachchan.
Mkongwe huyo alianza kuigiza filamu mwaka 1960, iliyoitwa Dil Bhi Tero Hum Bhi Teres, huku akiwa na nyota wengine, Balraj Sahni na Kum kum na mwaka uliofuata aliigiza filamu nyingine iliyojulikana kwa jina la Boy Friend.
Mwaka 1975, Dharmendra akiwa na Amitabh Bachchan, waliigiza pamoja filamu iliyoitwa Sholay ambayo hadi hivi leo filamu hiyo bado iko midomoni mwa wapenzi wa picha za Kihindi kutokana na ubora, matukio mengi ya kusisimua yaliyokuwa yakifanywa na wakongwe hao.
Kuanzia mwaka 1960 hadi 2013, Dharmendra amefanikiwa kuigiza filamu zaidi ya 300. Miongoni mwa zilizovuma na kumpatia umaarufu mkubwa licha ya Sholay ni Yaadon Ki Baaraat, Jugnu, Dost, Kartavya, Naseeb, Karishna Kudrat Kaa, Chupke Shupke, The Burning Train na Ghazab.
3. RISHI KAPOOR
Kapoor ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 64, naye ni miongoni mwa waigizaji wa filamu za Kihindi ambao wamejipatia umaarufu mkubwa. Filamu yake ya kwanza kuigiza ilikuwa ikiitwa Mera Naam Joker ambayo ilitoka mwaka 1970.
Filamu yake ya pili ambayo ilimjengea jina kubwa ilikuwa ikiitwa Bobby ambayo aliigiza mwaka 1973. Miongoni mwa waigizaji katika sinema hiyo ni Prem Chopra na Aruna Iran.
Mkongwe huyu amejipatia umaarufu mkubwa kutokana na aina yake ya uimbaji, kucheza miziki ya Kihindi na mara nyingine kuigiza kama haramia.
Miongoni mwa filamu zilizompatia umaarufu mkubwa mbali na Bobby ni Kabhie Kabhie, Hum Kisise Kum Naheen, Amar Akbar Anthony, Naseeb, Coolie na Laila Majnu. Katika kipindi cha miaka 46 kuanzia 1970 hadi 2016 ameigiza zaidi ya filamu 101.

No comments:

Post a Comment

Pages